• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa, na Rais wa Marekani watoa mwito wa kubadilishwa kwa urasimu umoja wa mataifa

  (GMT+08:00) 2017-09-19 08:59:57

  Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Antonio Geterres na Rais Donald Trump wa Marekani wametoa mwito wa kubadilishwa kwa urasimu kwenye umoja wa mataifa.

  Wakitoa maoni yao kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mageuzi ya Umoja wa mataifa, Bw Guterres amesema juhudi zinatakiwa kufanyika ili kubadilisha miundo na taratibu zinazofanya utendaji wa umoja wa mataifa usiwe na ufanisi. Amesema kwa sasa umoja wa mataifa unafanya mageuzi ya usimamizi ili kurahisisha utendaji wake.

  Rais Donald Trump amepongeza mtazamo wa Bw Guterres kuhusu mageuzi ya umoja wa mataifa na kusema urasimu na usimamizi mbaya umefanya umoja wa mataifa usiwe na utendaji wenye ufanisi. Bw Trump amesema tangu mwaka 2000, bajeti ya Umoja wa mataifa imeongezeka kwa asilimia 140 na wafanyakazi wake wameongezeka zaidi ya mara mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako