• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaongoza kwa kutoa mafunzo ya teknolojia na kusaidia kujiajiri

    (GMT+08:00) 2017-09-19 17:51:02

    Idara ya Teknolojia ya Juu iliyo chini ya Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya China imesema, maeneo zaidi ya 7,500 ya kutoa mafunzo na kujiajiri yameweza kuzalisha biashara zaidi ya laki mbili kwa mwaka jana.

    Idadi hiyo imeifanya China kuwa nchi inayoongoza kwa kutenga maeneo yenye wafanyakazi na vifaa na kutoza kodi ya chini kwa watu wanaoanzisha biashara pamoja na kutoa mafunzo hususan ya teknolojia na biashara.

    Takwimu hizo zimetolewa kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 30 tangu China ilipoanzisha kutenga maeneo hayo mwaka 1987 katika mji wa Wuhan mkoa wa Hubei.

    Mpango wa 15 wa miaka mitano wa Maendeleo ya China kwa mara ya kwanza umejumuisha mambo yatakayochochea kuendelea kwa kasi ya mfumo wa kuanzisha biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako