• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2017-09-19 18:17:54

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amekutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres huko New York katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

    Bw. Wang Yi amesema, China inautaka Umoja wa Mataifa uchukue nafasi kubwa zaidi wakati dunia inapokabiliana na changamoto nyingi za ukosefu wa amani na usalama. Kuhusu hali ya jimbo la Rakhine nchini Myanmar, Bw. Wang Yi amesema, China inapinga mashambulizi ya kimabavu katika eneo hilo, na inaunga mkono juhudi za Myanmar katika kulinda utulivu wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako