• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania kuanza kuuza nyama nje mwakani

    (GMT+08:00) 2017-09-19 18:22:33

    Tanzania itaanza tena kuuza nyama katika soko la kimataifa Januari mwakani wakati kiwanda cha nyama cha kisasa cha machinjio na usindikaji cha Nguru Hills kilichopo Mvomero, Morogoro kitakapoanza kazi.

    Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuchinja ng'ombe 300 na mbuzi 2,000 kwa siku. Ujio wa kiwanda cha Nguru unaleta matumaini mapya kwa sekta ya nyama baada ya Tanzania kutamba kati ya mwaka 1947 na 1975 kupitia kiwanda cha Tanganyika Packers Ltd (TPL) ambacho kilisafirisha nyama iliyosindikwa hadi soko la Ulaya.

    Wakati huo kiwanda hicho kilipokuwa kinafanya kazi kilikuwa ni kiwanda tanzu cha kampuni ya Uingereza ya kusindika nyama ya Liebig's Extract of Meat Corporation (Lemco). Kabla ya kutaifishwa mwaka 1974, TPL ilikuwa imeajiri watu 1,200.

    Tanzania ilipata pigo kubwa wakati Lemco walipoondoa chata yao katika leseni ya soko. Kuondolewa kwa leseni hiyo kulileta mgogoro mkubwa wa uzalishaji na mwaka 1993 kiwanda kilifungwa rasmi. Wakati TPL ikifanya kazi ilikuwa inachinja ng'ombe 550 kwa siku katika shifti mbili za kufanyia kazi.

    Kuanza kwa usindikaji huo katika kiwanda cha Nguru baada ya miaka 25 ya kuondoka katika soko la kimataifa kutasaidia ufugaji na wafugaji ambao kwa sasa wanalalamikia soko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako