• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema uzoefu wa taarifa ya pamoja ya "Septemba 19" bado una umuhimu mkubwa kwa suala la Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-09-19 21:00:30

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, uzoefu wa taarifa ya pamoja ya Septemba 19 iliyofikiwa katika miaka 12 iliyopita bado una umuhimu mkubwa kwa utatuzi wa suala la nyukilia la Korea ikilinganishwa na mchakato wa mabadiliko ya suala hilo na hali ya hivi sasa ya peninsula hiyo.

    Mwaka 2005 nchi sita husika zilifanya duru ya nne ya mazunguzo hapa Beijing na kutoa taarifa ya pamoja ya "Septemba 19". Kwenye taarifa hiyo, Korea Kaskazini iliahidi kuacha silaha zote za kinyuklia na mpango wake wa nyuklia, huku Marekani ikithibitisha kuwa haina kusudi la kuishambulia Korea Kaskazini kwa silaha za kawaida au za nyukila ama kuvamia nchi hiyo. Bw. Lu amesema, mambo hayo yalionesha makubaliano ya maslahi ya pande mbalimbali.

    Akizungumzia suala la nyuklia la Iran, Bw. Lu amethibitisha kuwa pande sita za suala hilo pamoja na Iran zitafanya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje ambao waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Wang Yi pia atahudhuria. Ameeleza kuwa mkutano huo utajadili maendeleo ya utekelezaji wa makubaliano ya pande zote ya suala la nyuklia la Iran na kutoa mwongozo wa kisiasa kwa utekelezaji wa baadaye wa makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako