• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan aonya dhidi ya biashara ya silaha kwenye mpaka kati ya Sudan na Chad

    (GMT+08:00) 2017-09-20 09:31:08

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan ameonya dhidi ya biashara ya silaha na kuhifadhi silaha kwenye mpaka kati ya Sudan na Chad.

    Onyo hilo amelitoa kwenye ziara yake iliyoanza jana katika jimbo la Darfur, ambalo limeshuhudia mapambano tangu mwaka 2003. Rais Al-Bashir amesisitiza kuwa mpaka huo haupo kwa ajili ya kuvusha silaha, bali kuingiza vitu vyenye manufaa. Pia amezungumzia ushirikiano wa vikosi vya Sudan na Chad, kuwa ni mfano kwenye ushirikiano miongoni mwa nchi zinazochangia mipaka. Awali, rais al-Bashir aliahidi kutekeleza mpango wa serikali wa kunyang'anya silaha huko Darfur na kuwataka wananchi kujitolea kukabidhi silaha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako