• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjadala kwenye mkutano wa 72 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2017-09-20 09:36:48

    Mjadala kwenye mkutano wa 72 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa umefunguliwa mjini New York, ambapo washiriki zaidi ya 100 watajadiliana kuhusu ufumbuzi wa matishio na changamoto zinazoikabili dunia.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw António Guterres ametoa taarifa ya kazi akieleza wasiwasi wake kuhusu changamoto na matishio yanayoikabili dunia, ikiwa ni pamoja na tishio la nyuklia, mabadiliko ya hali ya hewa, itikadi kali na ugaidi.

    Mwenyekiti wa mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bw Miroslav Lajcak, amesisitiza kuwa mkutano huo utaisaidia jumuiya ya kimataifa kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, na ahadi iliyotolewa kwa Makubaliano ya Paris.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako