• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei za bidhaa za kila siku zaongezeka wakati upungufu wa fedha za kigeni ukiendelea nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2017-09-20 19:26:55

    Bei za bidhaa za kila siku zinaendelea kuongezeka katika maduka wakati upungufu wa fedha za kigeni ukidumu, hivyo kuwalazimisha wafanyabiashara kupata dola za kimarekani kutoka masoko yasiyosajiliwa kwa gharama ya juu.

    Meneja wa ngazi ya kati kutoka maduka ya rejareja yanayoongoza nchini humo amesema, wafanyabiashara wanalipa gharama kubwa kuendelea kutoa bidhaa, na hawana chaguo lingine isipokuwa kuhamisha gharama hizo kwa wamiliki wa maduka, ambao ili kuhakikisha wanapata kiwango cha faida cha asilimia 10 katika bidhaa zinazotolewa, nao wanaongeza bei za bidhaa hizo.

    Mwanauchumi Bw. Clemence Machadu amesema, utoaji wa dola za kimarekani unaendelea kutokuwa imara kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo ongezeko la manunuzi kutoka nchi za nje, biashara za magendo na baadhi ya watu kuhifadhi fedha kwa ajili ya malengo maalumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako