• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liverpool yatupwa nje na Leicester City kombe la EFL

    (GMT+08:00) 2017-09-21 08:22:57

    Michezo ya EFL Cup imeendelea nchini England, na moja kati ya mchezo uliyochezwa juzi usiku ni kati ya Liverpool dhidi ya Leicester City uliyochezwa katika dimba la King Power. Leicester City wakiwa katika uwanja wao wa King Power wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Liverpool, magoli ya Leicester City yamefungwa na Shinji Okazaki dakika ya 66 na Islam Sliman dakika ya 78.

    Mabao hayo yalipatikana baada ya Liverpool kutawala kipindi cha kwanza ambapo Philippe Coutinho alikuwa amecheza vyema sana kabla ya kuondolewa uwanjani. Alex Oxlade-Chamberlain na Dominic Solanke walionunuliwa na Liverpool majuzi wote walipoteza nafasi nzuri za kufunga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako