• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajitahidi kutoka masomo na kozi za kimataifa

    (GMT+08:00) 2017-09-21 18:22:43

    Mamlaka nchini China zimezindua mradi unaolenga kupandisha ngazi ya vyuo vikuu 42 nchini humo kuwa vya ngazi ya kimataifa.

    Waraka wa pamoja uliotolewa na Wizara ya Elimu na Wizara ya Fedha pamoja na Tume ya Taifa ya Mageuzi na Maendeleo imesema, vyuo vingine 92 vimeandaliwa kuendeleza kozi za kimataifa. Mradi huo unajumuisha vyuo vikuu kadhaa vikiwemo Chuo Kikuu cha Peking, Chuo Kikuu cha Renmin cha China, na Chuo Kikuu cha Tsinghua. Waraka huo umesema, vyuo hivyo vilichaguliwa baada ya mchakato wa ushindani, kuangaliwa na wataalam, na tathmini iliyofanywa na serikali.

    Mradi huo mpya unatokana na miradi miwili ya awali na una lengo la kuboresha uratibu wa kikanda wa maendeleo ya elimu ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako