• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: MTN Rwanda yafuta ada ya asilimia 10 kwa huduma ya Me2U

    (GMT+08:00) 2017-09-21 18:30:56

    Kampuni ya kutoa huduma za mawasiliano ya MTN Rwanda imefuta ada ya asilimia 10 kwa huduma ya Me2U kufuatia malalamiko kutoka kwa wateja.

    Kaimu ofisa mkuu wa mauzo wa MTN Gaspard Bayigane amesema watarejesha pesa kwa wateja walioathirika.

    Huduma hiyo ya Me2U inawezesha wateja kutumiana pesa za kupiga simu lakini sasa kampuni hiyo imesema itatoa huduma hiyo bila malipo.

    Bayigane amesema pia huduma hiyo imeboreshwa na sasa mteja anaweza kutuma kati ya franc 100 na 20,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako