• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya yapokea mkopo wa bilioni 15.5 kufadhili usambazaji wa umeme maeneo kame

    (GMT+08:00) 2017-09-21 18:31:38

    Serikali ya Kenya imepokea mkopo wa shilingi bilioni 15.5 za kufadhili usambazaji wa umeme kwenye maeneo kame nchini humo.

    Pesa hizo zitatumika kununua vifaa vya kunasa kawi ya miale ya jua na kusambaza kwa nyumba 690,000

    Watakaonufaika wako kwenye kaunti 14 ambazo ziko kwenye maeneo kame.

    Katibu wa kudumu kwenye wizara ya kawi nchini humo Joseph Njoroge amesema mkopo huo utasaidia kampeni ya serikali ya kuunganisha watu zaidi na umeme ya Last Mile ifikapo mwka 2020.

    Amesema kwamza miradi itatekelezwa katika kaunti za Moyale, Garissa na West Pokot kabla ya kusambaza kwenye kaunti nyingine.

    Kwa sasa zaidi ya nyumba milioni 6.2 wameunganishwa na umeme na serikali inalenga kuunganisha milioni 1.7 zaidi katika kipindi hiki cha fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako