• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Neymar ataka hasimu wake Cavani auzwe

    (GMT+08:00) 2017-09-22 08:38:58

    Katika habari ambayo imegonga sana vichwa vya habari wiki hii ni ile ya mvutano kati ya mshambuliaji ghali duniani Neymar Dos Santos na mshambuliaji wa PSG Edison Cavanni.

    Na sasa kulingana na gazeti la Spanish Outlet Sport, mchezaji ghali zaidi duniani Neymar amemtaka mwenyekiti wa klabu hiyo Nasser Al-Khalifi kumuuzilia mbali mwenzake akisema kuwa uhusiano wake na Cavani umeharibika na hivyo basi hawawezi kucheza pamoja. Inaaminika kwamba Neymar anataka mshambuliaji huyo kuuzwa wakati wa kufunguliwa kwa dirisha la uhamisho mwezi Januari.

    Wafalme hawa wawili wameonekana kuvutana sana kuhusu nani atakayekuwa anapiga mipira ya adhabu karibu na lango la wapinzani na nani atakuwa akipiga penati. Edson Cavanni amekuwa mpiga penati wa PSG kwa muda mrefu sana lakini Neymar pia ameonekana na ujuzi wa penati na hata akiwa Barcelona alikuwa akipiga baadhi ya penati.

    Kocha wa PSG Unai Emery alipoulizwa kuhusu nani haswa ndio mpiga penati wao, alimalizia kwa kujibu mtu wa kwanza anayetakiwa kupiga penati katika timu yetu ni Cavanni na Neymar ndio anafuatia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako