• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti wa Marekani waonesha kuwa gharama ya kutafiti dawa mpya za kupambana na saratani ni za chini zaidi kuliko thathmini

    (GMT+08:00) 2017-09-22 17:51:26

    Dawa mpya za kupambana na saratani huwekwa bei ya juu sana, mashirika ya utengenezaji wa dawa yanatetea kuwa chanzo cha bei ya juu ya dawa hizo ni gharama kubwa ya utafiti. Lakini utafiti mpya uliotolewa na Marekani umesema, kubuni dawa mpya ya kupambana na saratani kunahitaji dola milioni 650 hivi za kimarekani, ambazo ni chini sana ikilinganishwa na takwimu zilizotolewa na shughuli ya utengenezaji wa dawa.

    Shughuli ya utengenezaji wa dawa husema, utafiti wa dawa mpya na utoaji wa dawa hizo unahitaji miaka kumi na milioni mia 100 za kimarekani. Mwaka 2014, taasisi ya dawa ya Tufts ya Marekani ilitoa taarifa ikisema, gharama ya kubuni dawa mpya ni kutoka dola milioni 800 za kimarekani hadi dola bilioni 2.6 za kimarekani.

    Ili kuhesabu gharama ya kubuni dawa mpya, watafiti kutoka chuo kikuu cha sayansi cha Oregon cha Marekani naTaasisi ya saratani ya Sloan-Kettering wametumia njia mpya kutafiti gharama za utafiti za kampuni 10, na kugundua kuwa muda wa wastani wa kuanzishwa kwa utafiti wa dawa mpya hadi kutolewa sokoni ni miaka 7.3 na gharama ya wastani ya utafiti ni dola milioni 648 za kimarekani.

    Watafiti wametoa taarifa ikisema, katika hali isiyoharibu uvumbuzi, bei za dawa zinaweza kupungua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako