• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu mpya wa Kenya Airways kuweka juhudi za kulikwamua shirika hilo

    (GMT+08:00) 2017-09-22 17:55:18

    Katibu mkuu mtendaji wa shirika la ndege la Kenya Bw Sebastian Mikosz ametangaza mpango wake wa kulikwamua tena shirika hilo ambalo limeendelea kupata hasara badala ya faida. Miskosz ambaye ameteuliwa hivi majuzi amesema atafanya maamuzi ambayo ni makali yanayolenga kuinua hadhi ya shirika hilo. Miskosz amechukua nafasi hiyo wakati ambapo shirika hilo lina zaidi ya deni la shilingi bilioni 150 na limekuwa likipata hasara kwa muda wa zaidi ya miaka mitano.Mkuu huyo ambaye ni raia wa Poland amesema hakuajiriwa na shirika hilo kumridhisha mtu binafsi bali ni kuweka mikakati itakayolifanya shirika hilo kupata mafanikio. Bodi ya shirika la ndege la Kenya lilihidhinisha uteuzi huo wa Sebastian. Hata hivyo kumekuwa na wasi wasi miongoni mwa wafanya kazi ambao wanaona huenda wakapoteza kazi wakati wa mchakato wa kutekeleza mipango mipya ya Bw Sebastian.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako