• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na waziri mkuu wa Somalia

    (GMT+08:00) 2017-09-22 18:49:36

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na waziri mkuu wa Somalia Bw. Hassan Ali Khaire huko New York.

    Bw. Khaire amesema, serikali ya Somalia inatilia maanani hadhi ya kimataifa ya China na mchango muhimu uliotolewa na China katika kuhimiza maendeleo ya Afrika. Ameyataka mashirika ya China kuwekeza nchini Somalia na kuisaidia nchi hiyo kujenga miundombinu, kuendeleza uchumi na kutoa nafasi nyingi zaidi za ajira. Amesema Somalia inaunga mkono pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na inataka kutumia nguvu bora ya kijiografia kutoa mchango wa kipekee katika mchakato wa ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Bw. Wang amesema, China inaunga mkono serikali mpya ya Somaliakuchukua njia ya kujiendeleza yenye amani. Amesema China inapenda kushirikiana na Somalia kupitia njia za pande mbili, baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika na baraza la ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu, ili kuisaidia nchi hiyo kulinda amani, kuendeleza uchumi, kuboresha maisha ya watu na kuongeza uwezo wa kujiendeleza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako