• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani asaini amri ya kuimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-09-22 18:50:11

    Rais Donald Trump wa Marekani amesaini amri inayolenga kuzidisha eneo la vikwazo vilivyowekwa na wizara ya fedha ya Marekani dhidi ya Korea Kaskazini.

    Rais Trump amesema hayo alipohudhuria mkutano na viongozi wa Japani na Korea Kusini huko New York. Kwa mujibu wa amri hiyo mpya, wizara ya fedha ya Marekani itakuwa na madaraka ya kuweka vikwazo dhidi ya mtu yeyote na shirika lolote vinavyofanya biashara na Korea Kaskazini pamoja na mashirika ya kifedha yanayosaidia kuhimiza biashara husika.

    Waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin amesema, amri mpya imeongeza idhini ya kuweka vikwazo ya wizara hiyo, kama benki za kigezi zikifanya biashara husika au kusaidia kuhimiza biashara hizo na Korea Kakazini katika hali ya kufahamu hali halisi, biashara zote kupitia akaunti zao nchini Marekani zitasimamishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako