Ikulu ya Marekani imetoa taarifa kuhusu mazungumzo kati ya marais wa Marekani na Korea Kusini yaliyofanyika Alhamisi kuwa, marais hao wawili walisisitiza kuwa nchi hizo mbili zinatafuta kwa pamoja njia ya kuihimiza Korea Kaskazini iache silaha za kinyukilia kwa njia ya amani. Pia wanaona kuwa, ili kuizuia Korea Kaskazini kuchukua hatua za kutishia na kuihimiza iache silaha za kinyukilia, ni lazima kuiwekea vikwazo kadiri iwezekanavyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |