• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege za Marekani zapitia eneo la bahari na anga ya Korea ya Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-09-24 17:36:13

    Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuwa, ndege nyingi za mashambulizi ya kimkakati za jeshi hilo zimepitia eneo la bahari na anga ya Korea ya Kaskazini zikilindwa na ndege za kivita.

    Msemaji wa wizara hiyo Bibi Dana White amesema kwenye taarifa moja kuwa, ndege za jeshi la angani la Marekani aina ya B-1B zilifika eneo hilo kutoka kituo cha kijeshi cha Marekani huko Guam. Pia imesema eneo hilo liko umbali mkubwa zaidi kaskazini mwa eneo la salama lililoko kati ya Korea ya Kusini na ya Kaskazini kwa ndege za jeshi la Marekani kufika tokea karne ya 21, hatua ambayo imeonesha utiliaji mkazo mkubwa wa Marekani kwa kitendo cha kichochezi cha Korea ya Kaskazini, pia inaonesha kuwa rais Trump wa Marekani ana machaguo mengi ya kukabiliana na tishio la Korea ya Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako