• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mshambuliaji wa kanisa jimboni Tennessee atambuliwa

    (GMT+08:00) 2017-09-25 09:05:04

    Polisi nchini Marekani wamesema mshambuliaji aliyefyatulia risasi katika kanisa moja jumapili katika jimbo la Tennessee, kusini mwa Marekani, ametambuliwa. Polisi wamesema mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 25 anayetambuliwa kwa jina la Emanuel Kidega Samson, ni mkazi halali wa Marekani aliyehamia nchi hiyo kutoka Sudan mwaka 1996, na alimwua kwa kumpigia risasi mwanamke mmoja kanisani, kusini mashariki mwa Nashaville. Kwa mujibu wa polisi, mshukiwa huyo ambaye pia alijeruhiwa kidogo ameruhusiwa kutoka hospitali na atakabiliwa na mashtaka ya mauaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako