• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkuu wa jimbo la Wakurdi athibitisha upigaji kura utaendelea leo

  (GMT+08:00) 2017-09-25 09:58:38

  Waziri Mkuu wa Iraq Hadar al-Abadi ameendelea kupinga upigaji kura za maoni za kujitenga kwa jimbo la Wakurdi zinazotarajiwa kufanyika leo.

  Bw Abadi ameonya kuwa kura hizo zitasababisha matatizo zaidi ikiwemo kuvunja umoja wa watu wa Iraq na kanda nzima, na kwamba ni kinyume na sheria na katiba.

  Mkuu wa jimbo la Wakurdi Bw Masoud Barzani amethibitisha kuwa upigaji kura utaendelea leo na hawatarudi nyuma, kwani wamefikia hitimisho kuwa kujitenga kutawafanya wasirejee tena kwenye madhila yaliyowakumba katika siku nyuma. Bw Barzani anatarajia kuwa Uturuki ambayo inapinga vikali kura hizo za maoni, haitafungua mpaka wake na Iraq, akionya kuwa pande zote mbili zinaweza kuathirika.

  Habari zaidi zinasema Iran imezuia ndege zake zote zinazokwenda na kutoka jimbo la Wakurdi baada ya kuombwa na serikali ya Iraq. Jana Uturuki pia ilifunga anga yake kwa ndege za Wakurdi. Iraq, Iran na Uturuki zimekubaliana kuchukua hatua kali kama jimbo hilo litapiga kura za maoni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako