• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Muungano wa vyama vya  CSU na CDU wa Ujerumani wapata kura nyingi zaidi kwenye uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-09-25 10:08:32

    Matokeo ya awali yaliyotolewa na mashirika mbalimbali yanaonyesha kuwa, muungano wa vyama vya CSU na CDU unaoongozwa na chansela Angela Merkel umepata kura nyingi zaidi kwenye uchaguzi mkuu wa Ujerumani.

    Matokeo yaliyotolewa jana usiku na televisheni ya Ujerumani yanaonyesha kuwa, muungano huo umepata asilimia 32.9 ya kura, ukifuatiwa na chama cha SPD ambacho kimepata asilimia 20.8 ya kura.

    Bibi Merkel amesema chama chake kimetimiza lengo la kimkakati, lakini amesema matokeo ya uchaguzi yangeweza kuwa mazuri zaidi.

    Kiongozi wa chama cha SPD Bw. Martin Schulz amesema, matokeo ya sasa yanasikitisha, chama chake hakikupata uungaji mkono wa kutosha, kwa hiyo hakikutimiza lengo lake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako