• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakurdi nchini Iraq waanza kupiga kura ya kihistoria ya maoni kutaka uhuru

  (GMT+08:00) 2017-09-25 18:12:58

  Wakurdi nchini Iraq leo wamepiga kura ya maoni ambayo itaamua uhuru wa mkoa a Kurdi na maeneo mengine ambayo yanakaliwa na jeshi lililoasi la Wakurdi.

  Watu milioni 5.2 wanaostahili kupiga kura katika mikoa mitatu ya Erbil, Sulaimaniyah na Dohuk, na maeneo mengine nje ya eneo hilo wanatarajiwa kupiga kura katika vituo elfu 12 vya kupigia kura vilivyowekwa kwenye eneo zima la Wakurdi na maeneo hayo. Wapiga kura wanatarajiwa kuchagua kama wanataka kuanzisha nchi huru ya Kikurdi au kubaki kama mkoa wenye utawala maalum ndani ya Iraq.

  Serikali ya Iraq imekataa kufanyika kwa kura hiyo na matokeo yake, ikielezea kuwa ni kinyume na katiba. Waziri mkuu wa nchi hiyo Haider al-Abadi amesema uamuzi huo utaathiri umoja wa Iraq, na upande mmoja kuamua kujitenga ni kinyume na sheria na katiba ya nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako