• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atembelea maonesho ya mafanikio yaliyopatikana nchini China katika miaka mitano iliyopita

  (GMT+08:00) 2017-09-25 20:35:10

  Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni rais wa China Xi Jinping ametembelea maonesho ya mafanikio yaliyopatikana nchini China katika miaka mitano iliyopita katika jumba la maonesho hapa Beijing, ikiwa ni siku chache kabla ya Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China kufanyika.

  Rais Xi amesema katika miaka mitano iliyopita, kamati kuu ya chama ikiongoza chama, nchi nzima na makabila mbalimbali, imesukuma mbele maendeleo ya ujamaa wenye umaalum wa China, kuboresha maisha ya watu, na shughuli za chama na nchi zimepata mafanikio na mageuzi ya kihistoria. Amesema Wachina wataendelea kufanya juhudi ili kutimiza ndoto ya kustawisha taifa la China, na kukaribisha ufunguzi wa mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako