• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanaume walikaa nyumbani huku wanawake wakihamahama huko Ulaya katika zama mpya ya mawe

  (GMT+08:00) 2017-09-25 21:10:11

  Watafiti wa Ujerumani wamegundua kuwa mwishoni mwa zama mpya za mawe barani Ulaya, wanaume walikaa nyumbani huku wanawake wakihamahama, na wanawake waliohamahama huenda walitoa mchango mkubwa kwa mawasiliano ya kiutamaduni kati ya sehemu mbalimbali na kusaidia binadamu kuingia zama ya shaba nyeusi.

  Taasisi ya historia ya binadamu ya Max Planck ya Ujerumani imetoa ripoti ikisema watafiti wa taasisi hiyo na idara nyingi wametafiti mabaki ya mifupa ya miili 84 yaliyozikwa katika vijiji kadhaa vya zama za kale, na kugundua kuwa wanakijiji wa kiume ni wenyeji wa vijiji hivi, lakini wanawake walitoka sehemu mbalimbali.

  Vijiji hivi vilivyoko katika bonde la mto Lei lenye ardhi yenye rutuba nyingi kusini mwa jimbo la Bavaria la Ujerumani. Miili hiyo ilizikwa kati ya mwaka 2500 K.K hadi mwaka 1650 K.K. Upimaji wa DNA ya Mitochondria unaonesha kuwa wanawake wa vijiji hivi walitoka sehemu nyingi zikiwemo sehemu ya katikati ya Ujerumani au Bohemia, tena walihamia vijijini baada ya kuwa watu wazima. Wanawake hao walizikwa kwa njia sawa na wenyeji, ambayo inaonesha kuwa wamekubaliwa na wenyeji.

  Hali hii ya kuhama kwa wanawake iliendelea kwa miaka 800. Watafiti wamesema wanawake walipoolewa na wanaume wa vijiji vya mbali walileta vitu, desturi na mawazo mapya, na ni muhimu kwa mawasiliano ya kiutamaduni kati ya sehemu mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako