• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Shirikisho Afrika: TP Mazembe yatinga nusu fainali kwa kufanya mauaji dhidi ya waarabu.

    (GMT+08:00) 2017-09-26 08:43:34

    Mabingwa watetezi wa kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya TP Mazembe ya DRC imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Shirikisho baada ya kuwatandika Waarabu wa Sudan, Al-Hilal Obeid kwa mabao 5-0 na kuwatupa nje kwa jumla ya magoli 7-1.

    TP Mazembe wakiwa kwenye dimba lao la Stade Fredric Kibassa Maliba lilipo Mjini Lubumbashi waliingia uwanjani wakiwa na ushindi magoli 2-1 ambao waliupata Sudan wiki iliyopita.

    Kwa Matokeo hayo TP Mazembe wametinga hatua ya Nusu Fainali la Shirikisho barani Afrika huku wakisaka nafasi ya kuchukuwa kombe hilo kwa mara ya pili Mfululizo ikumbukwe hao ndo mabingwa watetezi na watakutana na timu ya FUS Rabat ya Morocco ambao nao walitinga Nusu baada ya kuwachapa Watunisia timu ya CS Sfaxien kwa jumla ya mikwaju 4-3 ya Penalti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako