• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping azungumza na waziri mkuu wa Uingereza kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2017-09-26 09:15:28

    Rais Xi Jinping wa China jana alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May kuhusu ushirikiano kati ya pande mbili.

    Katika mazungumzo yao, rais Xi alikumbusha mkutano wa Kundi la nchi 20 uliofanyika mwezi Julai mjini Hamburg Ujerumani, ambapo yeye na Bibi May walikubaliana kuimarisha ushirikiano na kuendelea kujenga uhusiano kati ya nchi zao. Rais Xi ameongeza kuwa nchi hizi mbili zikiwa zinatimiza miaka 45 ya uhusiano wao wa kibalozi zinapaswa kuimarisha mawasiliano kati ya pande mbili, kuendeleza majadiliano kati ya taasisi mbalimbali, kuhusu kuendeleza kasi ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara, utamaduni, kuimarisha mafungamano ya mikakati ya maendeleo kati ya nchi mbili ndani ya pendekezo la Ukanda mmoja njia moja, na kuimarisha ushirikiano katika kulinda amani ya dunia na maendeleo.

    Bibi May amesema Uingereza inaona kuna umuhimu mkubwa wa kukuza uhusiano na China, na kwamba iko tayari kushirikiana nayo katika mambo ya uchumi, biashara, usalama na utamaduni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako