• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping ahimiza kuunda jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu wote

    (GMT+08:00) 2017-09-26 17:55:22

    Mkutano mkuu wa Shirika la Polisi la Kimataifa Interpol umefunguliwa leo hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China amehudhuria na kuhutubia mkutano huo, akihimiza pande mbalimbali kuunda jumuiya yenye mustakabali wa pamoja inayoweza kuhakikisha usalama wa binadamu wote, na kutoa mapendekezo kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano wa usalama wa utekelezaji wa sheria duniani.

    Ikiwa ni shirika kubwa la pili kati ya serikali za nchi mbalimbali duniani baada ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Polisi la Kimataifa Interpol linafanya kazi zisizoweza kufanywa na mashirika mengine katika kukuza ushirikiano wa kimataifa wa shughuli za polisi, na kupambana kwa ufanisi na uhalifu wa kijinai wa kuvuka mipaka vikiwemo vitendo vya ugaidi, dawa za kulevya, na magendo. Mkutano huo umehudhuriwa na wanasheria kutoka nchi 158 na wajumbe wa mashirika yanayohusika ya kimataifa. Kwenye hotuba yake, rais Xi Jinping ameeleza kuwa, hivi leo dunia bado haijawa na usalama wa kudumu, masuala ya usalama yakiwemo ugaidi, uhalifu kupitia mtandao wa Internet, na uhalifu wa kuvuka mipaka yanaleta wasiwasi siku hadi siku, na matishio ya usalama yanaibuka moja baada ya lingine, ambapo binadamu wanakabiliwa na changamoto nyingi za pamoja.

    "Masuala ya usalama yamezidi kuhusiana, kuathiri nchi nyingi na kuwa na aina nyingi. Hayo ni masuala muhimu yanayohusu mustakabali wa binadamu wote. Kuwepo kwa amani na maendeleo kunahitaji kuhakikisha kwanza usalama na utulivu, ama sivyo hazipatikani kamwe. China inapenda kushirikiana na serikali na idara za sheria za nchi mbalimbali na mashirika ya kimataifa, kuongeza ushirikiano katika mambo ya polisi na usalama kwa kufuata kanuni ya ushirikiano, uvumbuzi, utawala wa sheria na mafanikio ya pamoja, ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja inayoweza kuhakikisha usalama wa binadamu wote."

    Rais Xi ametoa mapendekezo kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano wa usalama wa utekelezaji wa sheria duniani, na kusisitiza kuwa ushirikiano huo unapaswa kufuata kanuni ya ujenzi wa pamoja kwa ushirikiano, mageuzi na uvumbuzi, moyo wa sheria, na kunufaishana na mafanikio ya pamoja. Amependekeza nchi mbalimbali kuwa na mawazo endelevu ya pamoja na ya jumla yanayozingatia ushirikiano kuhusu usalama wa dunia, kugeuza na kukamilisha mfumo wa utawala wa kimataifa, kushikilia na kulinda kanuni za Umoja wa Mataifa na Shirika la Polisi la Kimataifa , na kuunga mkono zaidi nchi zinazoendelea katika shughuli za usalama na maendeleo.

    Rais Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya China imesukuma mbele ujenzi wa usalama na utawala wa sheria, na kuendeleza mfumo na uwezo wa utawala wa jamii kuwa wa kisasa.

    "Kuwapatia wananchi mazingira mazuri ya maisha yenye usalama na utulivu ni lengo kuu la utawala wa serikali ya China. Hivi leo jamii ya China ina utulivu na utaratibu, huku wananchi wakiishi maisha bora. Watu wengi duniani wanaona China ni moja ya nchi zenye usalama zaidi duniani. Huu ni mchango uliotolewa na China kwa ajili ya juhudi za kudumisha usalama na utulivu duniani. Aidha mbali na kushughulikia vizuri mambo ya ndani, China pia imetekeleza wajibu wa kimataifa kwa makini, na kushiriki na kutetea ushirikiano wa kimataifa wa kutekeleza sheria na shughuli za usalama duniani. China inapenda kutoa uzoefu wake kuhusu shughuli za usalama kwa nchi nyingine, ili kuchangia juhudi za kudumisha usalama duniani."

    Rais Xi amesema serikali ya China itaunga mkono zaidi operesheni za Shirika la Polisi la Kimataifa katika miaka mitano ijayo. Anasema,

    "Mustakabali wa binadamu ni mzuri, lakini haupatikani bila ya kufanya juhudi. Binadamu wote wanapaswa kufanya jitihada za pamoja. Mchakato wa amani na maendeleo pia hautakuwa shwari, nchi zote duniani zinapaswa kufanya juhudi za pamoja ili kutimiza lengo la kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja. China inapenda kushirikiana na pande zote, ili kutoa mchango zaidi kwa ajili ya kuhimiza amani na maendeleo duniani. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako