• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa mahindi walalamika kuendelea kuwepo na unga wa bei rahisi

    (GMT+08:00) 2017-09-26 19:03:37

    Wakulima wa mahindi nchini Kenya wamelalamika kwamba kuendelea kuwepo na unga uliopunguzwa bei na serikali kutaathiri soko.

    Chama cha wapanzi wa nafaka nchini humo kinadai kuwa sasa bei ya gunia moja la mahindi la kilo 90 imepungua hadi dola 23 ikiwa ni ya chini ikilinganishwa na bei za awali.

    Wiki iliopita waziri wa kilimo Willy Bett alitangaza kwamba serikali itaendelea kutoa punguzo la bei kwa unga wa mahindi ambao sasa unauzwa kwa shilingi 90 kwa kilo mbili.

    Alisema hatua hiyo inatokana na kwamba bado Kenya haina mahindi ya kutosha baada ya mvua nyingia kuathiri mavuno.

    Alisema mahindi ya kwanza yanatarajiwa sokoni baadaye mwezi Oktoba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako