• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Hisa za TBL zaendelea kufanya vyema

    (GMT+08:00) 2017-09-26 19:04:21

    Licha ya kutangaza kushuka kwa faida yake kutokana na kupigwa marufuku kwa pombe za viroba, wawekezaji wameendelea kuwa na imani na hisa za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) hivyo kuongoza kwa mauzo kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) wiki iliyoishia.

    Kwa wiki iliyoishia Septemba 22, mauzo yalifika Sh53.5 bilioni yakiongezeka kwa takriban mara 10 kutoka Sh5.4 bilioni yaliyopatikana wiki iliyoishia Septemba 15. Mauzo hayo yalichangiwa na ongezeko la hisa kutoka milioni mbili mpaka milioni 4.4 ndani ya muda huo.

    TBL ilikuwa kinara baada ya kuuza asilimia 99 ya hisa zote zilizonunuliwa sokoni hapo, ikifuatiwa na Kampuni ya Vodacom iliyouza asilimia 0.22 na Benki ya CRDB ikifunga pazia hilo kwa kuuza asilimia 0.09.

    Licha ya kuchangia kwenye mauzo ya soko, TBL ilifanya hivyo kwenye ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani ulioongezeka kwa Sh27 milioni na kufika Sh9.67 trilioni wiki hiyo, kutokana na kupanda kwa bei ya hisa zake kwa asilimia 0.75 hivyo kuuzwa kwa Sh13,400 kila moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako