• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashindano ya kuogelea kanda ya tatu ya Afrika (CANA ZONE 3) kuanza Oktoba

    (GMT+08:00) 2017-09-27 09:23:10

    Mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu ya Afrika (Cana zone 3) yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 19-21 ambapo nchi mbalimbali zimezidi kuthibitisha ushiriki wao.

    Rwanda na Sudan zimethibitisha kushiriki michuano hiyo zikiungana na nchi nyingine 6 zilizothibitisha kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Chama Cha kuogelea nchini (TSA), Leena Kapadia.

    Kapadia amezitaja nchi hizo kuwa ni Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Uganda, Djibouti na wenyeji Tanzania huku zaidi ya waogeleaji 200 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo ambayo Tanzania ni mabingwa watetezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako