• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kushirikiana na Marekani ili kuhakikisha ziara ya rais wa Marekani nchini China inafanikiwa

    (GMT+08:00) 2017-09-27 18:46:27

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson atafanya ziara nchini China mwishoni mwa mwezi huu, ili kufanya maandalizi ya ziara rasmi ya rais Donald Trump nchini China itakayofanyika baadaye mwaka huu.

    Msemaji huyu amesema China inapenda kudumisha mwelekeo wa mawasiliano na ushirikiano na Marekani, kushirikiana na nchi hiyo kuhakikisha ziara ya rais Trump inafanikiwa, na kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika kipindi kipya.

    Lu Kang amesema, katika ziara ya Bw. Tillerson, China na Marekani zitabadilishana maoni kuhusu masuala makubwa ya kimataifa na ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako