• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ugonjwa wa Parkinson unaweza kutambuliwa kupitia uchambuzi wa uwezo wa kuchora

  (GMT+08:00) 2017-09-28 14:47:15

  Je, ugonjwa wa Parkinson unaweza kutambuliwa kupitia kuchora mstari wa kuzunguka kwenye karatasi? Watafiti wa Chuo Kikuu cha RMIT cha Australia wamebuni software moja inayoweza kutambua ugonjwa huo kupitia uwezo wa kuchora, ambayo kiwango cha usahihi kinaweza kufikia asilimia 93.

  Ugonjwa wa Parkinson ni ugonjwa unaoathiri polepole mfumo wa neva ya kati. Watu wenye ugonjwa wa Parkinson, polepole hupoteza uwezo wa kudhibiti kabisa harakati za vitendo vya mwili.

  Utafiti wa awali umegundua kuwa wagonjwa wenye hali mbaya wa Parkinson wanapochora, nguvu na kasi inaweza kupungua. Watafiti wa chuo kikuu hicho wamebuni software kutokana na msingi huo, ambayo inaweza kuweka kumbukumbu na kutafiti kasi na nguvu ya kalamu wakati watumiaji wanapochora mstari wa kuzunguka, ili kutambua ugonjwa huo na hali ya ugonjwa.

  Watafiti wamesema, software inaweza kutambua ugonjwa huo kabla ya mgonjwa kuonesha dalili za ugonjwa, ambayo inaweza kusaidia kutibu mapema. Wamesisitiza kuwa wakati wa kuanza tiba ya ugonjwa wa Parkinson ni muhimu sana, kwa kuwa kama wagonjwa wakionesha dalili za kutetemeka, utoaji wa tiba unakuwa umechelewa.

  Imefahamika kwamba, matumizi ya software hiyo ni rahisi sana, watafiti wanataka teknolojia hiyo iweze kutumiwa kwenye upimaji wa ugonjwa wa Parkinson, ili kugundua hali ya ugonjwa mapema zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako