• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maisha mazuri ya mlinzi wa mazingira ya asili wa eneo la chanzo cha mito mitatu nchini China

  (GMT+08:00) 2017-09-28 18:38:41

  Bw. Zhaxi Cairen mwenye umri wa miaka 28 ni mfugaji aliyezaliwa na kukua katika eneo la ufugaji la mto wa Tuotuo ambao ni chanzo cha mto wa Changjiang. Mwezi wa Agosti, yeye na walinzi wengine wawili wa mazingira ya asili wamebeba mahitaji ya kila siku ikiwemo hema na chakula kuendesha gari kwa umbali wa kilomita 500 kurudi katika kando ya mto wa Tuotuo, ili kufanya doria katika mbuga yenye baridi ambayo ufugaji umepigwa marufuku katika miaka zaidi ya kumi iliyopita.

  Hii ni mara ya pili kwa Bw. Zhaxi kwenda eneo la mto wa Tuotuo tangu ashirki kwenye doria ya pamoja mwezi wa Aprili mwaka huu. Ameendesha gari kwa umbali wa kilomita 420 na kufika wilaya ya Tanggulashan yenye urefu wa mita 4500 kutoka usawa wa bahari na kupanda mpaka mbuga ya chanzo cha mto wa Tuotuo yenye urefu wa mita 4800 kutoka usawa wa baahari. Kama walinzi wengine wa mbuga kutoka kijiji cha Chang Jiangyuan, kila doria aliyofanya Bw. Zhaxi hutumia zaidi ya siku tatu na umbali zaidi ya kilomita 1000. Akiwa mmoja kati ya walinzi wa mbuga wa kundi la kwanza kijijini, kila mwaka Bw. Zhaxi anashiriki kwenye shughuli hiyo ya doria. Anasema,

  (Sauti 2)

  "Mshahara wa walinzi wa mazingira ya asili sio juu, unatakiwa kujaza mafuta kwenye gari ili kuendesha kwa umbali wa kilomita 400 kufika wilaya ya Tanggulashan. Baada ya kupanda mlima, utatakiwa kukodi pikipiki, matumizi ni mengi. Lakini mshahara kuwa juu au la si swali muhimu, kulinda mazingira ya asili na mbuga ni jukumu hilo, hivyo ninatakiwa kutekeleza jukumu langu."

  Mwaka 2004, kutokana na sera ya ulinzi wa chanzo cha mto wa Changjiang, wafugaji 407 maskini wameondoka mbuga hiyo na kushuka kutoka mlima wa Tanggula na kuhamia kijiji cha Changjiangyuan kilichoko katika kitongoji cha mji wa Geermu. Katika miaka zaidi kumi iliyopita, idadi ya wakazi wa kijiji hicho imeongezeka hadi 578, huku hali ya maisha ikiboreka na pato la wastani la mtu likiongezeka kutoka dola 300 za kimarekani hadi dola 3000 za kimarekani. Katika miaka zaidi ya kumi iliyopita, mabadiliko makubwa zaidi katika mbuga hiyo ni kuwa majani yamekua vizuri zaidi na wanyama wengi wa porini wameonekana tena katika mbuga hiyo.

  Ingawa mshahara wa mlinzi wa mazingira ya asilini sio mwingi, lakini baba wa Zhaxi Bw. Shen Ge mwenye umri wa miaka 57 anaona kuwa ni heshima yao ambayo wanaweza kurudi mbuga ambayo mababu wao walilisha mifugo. Bw. Shen Ge anasema,

  (Sauti 3)

  "Ulinzi wa mazingira ya kiasili ya mbuga ni jukumu kubwa zaidi la wafugaji. Ingawa tumehama, lakini mioyo yetu bado iko katika mbugani, kwa sababu watu wanaotoka mbuga hawawezi kusahau mbuga hiyo. Ninawaambia watoto mara kwa mara kuwa tunatakiwa kulinda mbuga kama maisha yatu. Kama hakuna mbuga wala milima au misitu, hakutakuwa na maisha ya wafugaji. Kulinda mazingira ya asili ni kulinda ng'ombe na mbuzi wetu na kulinda maisha yetu."

  Kazi za walinzi wa mazingira ya asili ya mbuga ni pamoja na kusaidia idara za usimamizi wa mbuga kufanya doria katika mbuga na kuripoti vitendo vya uhalifu. Walinzi hao wanaajiriwa kila baada ya mwaka mmoja, huku wakiweza kurefusha mikataba baada ya kupita ukaguzi. Kila mwaka walinzi hao wanaweza kupata pato la dola 3239 za kimarekani kila mwaka. Mwaka 2016, serikali ya China imetekeleza duru mpya ya ruzuku kwa walinzi hao, na kuunganisha mfumo wa walinzi wa mazingira ya asili na sera ya kusaidia watu maskini katika mbuga ya ufugaji na kuongeza nafasi za ajira za walinzi hao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako