• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Tanzania yahimiza kilimo cha pamba

    (GMT+08:00) 2017-09-28 18:45:46

    Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa 11 inayolima pamba nchini wahakikishe wanasimamia vizuri wakulima wa zao hilo ili kuongeza uzalishaji na kuwaletea tija wananchi.

    Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu wakati akizungumza na wakuu hao wa mikoa kwenye kikao alichokitiisha mjini Dar es Salaam kujadili maendeleo ya zao hilo.

    Waziri Mkuu amesema katika kipindi hiki ambacho msimu wa maandalizi ya kilimo cha pamba umeanza ni vema kwa Maofisa Kilimo na Wagani wakawasimamia wakulima kwa ukaribu ili wahakikishe wanafuata mbinu bora za kilimo.

    Amesema iwapo wakulima watapata usimamizi mzuri kutoka kwa Maofisa Ugani waliopo kwenye maeneo yao kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba yao itawasaidia katika kuongeza tija, kwenye uzalishaji wao.

    Amesema Maafisa Kilimo wote walioko kwenye kila Halmashauri ni lazima wahusike kikamilifu katika kuwaelekeza wakulima namna ya kutumia mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi.

    Pia Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Vyuo vya Kilimo nchini wahakikisha wanakuwa na mashamba darasa yatakayotumika na wakulima na wanafunzi wao kujifunza mbinu bora za kilimo kwa vitendo.

    Wakuu wa mikoa walioitwa kwenye kikao hicho ni kutoka mikoa ya Shinyanga, Singida, Kagera, Tabora, Morogoro, Mara, Mwanza, Simiyu, Katavi, Kigoma na Geita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako