• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Wadau wa biashara ya uchukuzi waitisha huduma za saa 24

    (GMT+08:00) 2017-09-28 18:45:46

    Washikadau katika sekta ya uchukuzi wamelaumu oparesheni za biashara katika mpaka wa Uganda-Rwanda wakisema zinachelewesha mizigo yao.

    Licha ya kuanza kutumika kwa sheria mpya ya ukaguzi wa kituo kimoja ,shughuli ya biashara katika mpaka huo zimesalia chache.

    Wadau hao sasa wamependekeza matumizi ya saa 24 ya kazi badala ya saa 12 .

    Moses Sabiiti mkurugenzi wa halmashauri ya barabara nchini Uganda amesema utaratibu mpya utakaowekwa wa saa 24 pamoja na matumizi ya barabara mpya ya kilomita 37 ya katuna hadi Gatuna yataboresha huduma za biashara.

    Upande wa muungano wa wamiliki wa viwanda umetoa mwito wa kuharakishwa kwa upakuaji wa mizigo kutoka banadarini .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako