• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atoa heshima kwa mashujaa wa taifa katika Uwanja wa Tian'anmen

  (GMT+08:00) 2017-09-30 18:51:28

  Rais Xi Jinping wa China na viongozi wengine wa ngazi ya juu wametoa heshima na kuweka mashada ya maua kwenye mnara wa Mashujaa wa China ulioko kwenye Uwanja wa Tian'anmen hapa Beijing.

  Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, ameungana na wawakilishi kutoka nyanja zote kuadhimisha Siku ya Mashujaa, ikiwa ni siku moja kabla ya Siku ya Taifa la China, Oktoba Mosi.

  Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China akiwemo Li Keqiang, Zhang Dejiang,Yu Zhengshen, Liu Yunshan, Wang Qishan na Zhang Gaoli pia walihudhuria hafla hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako