• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaadhimisha siku ya kitaifa

    (GMT+08:00) 2017-10-01 18:41:28

    China leo imefanya shughuli mbalimbali ili kuadhimisha miaka 68 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

    Baraza la serikali ya China leo limeandaa tafrija ya kuadhimisha siku hiyo, ambayo imehudhuriwa na rais Xi Jinping, waziri mkuu Li Keqiang, na viongozi wengine wengi wa China.

    Zaidi ya watu 115,000 kutoka maeneo mbalimbali nchini humu leo wamekusanyika katika Uwanja wa Tian'anmen kutazama kupandishwa kwa bendera ya Taifa.

    Siku ya kitaifa ya China inaadhimishwa kwa mapumziko ya wiki moja, wakati sikukuu ya mbalamwezi ambapo familia hukusanyika pamoja itasherehekewa. Inatarajiwa kuwa idadi ya watu watakaofanya utalii katika siku hizo za mapumziko itazidi milioni 710, na kati yao milioni sita watakwenda nchi za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako