• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Wang Yi afanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson

    (GMT+08:00) 2017-10-01 19:11:10
    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana hapa Beijing alifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson

    Bw. Wang Yi alisema kuwa, chini ya uongozi wa kimkakati wa rais Xi Jinping wa China na rais Donald Trump wa Marekani, uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulipata maendeleo makubwa, na kuwa na fursa muhimu ya kuhimizwa zaidi. Pande hizo mbili zinapaswa kujiandaa vizuri ili kuhakikisha ziara ya rais Trump kwa mwaliko wa rais Xi Jinping ipate mafanikio, na kuongeza nguvu mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Bw. Tillerson alisema kuwa, Marekani inazingatia uhusiano kati yake na China, na inapenda kupanua mawasiliano na ushirikiano na China katika sekta mbalimbali. Rais Trump anatarajia kufanya ziara nchini China na kupanga mustakabali ya maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na rais Xi Jinping.

    Pande hizo mbili pia zilibadilishana maoni kuhusu hali ya peninsula ya Korea na suala la Afghanistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako