• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chama cha Kikomunisti cha China chapata mafanikio katika kutimiza utawala bora

  (GMT+08:00) 2017-10-02 16:12:55

  Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimepata mafanikio makubwa katika kutimiza utawala bora.

  Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama hicho uliofanyika mwaka 2012, Kamati Kuu ya CPC imejidhatiti katika usimamizi bora wa chama, na katika miaka mitano iliyopita, Kamati hiyo imekabiliana bila kuchoka na aina nne za maadili mabovu ndani ya chama, ambayo ni mazoea, ukiritimba, anasa, na ubadhirifu.

  Kamati ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC imesema, mpaka kufikia mwisho wa mwaka jana, kesi zaidi ya laki moja kuhusu ukiukaji wa kanuni nane za matumizi zilichunguzwa.

  CPC pia imeongeza mapambano yake dhidi ya rushwa, ikilenga wala rushwa wakubwa na wadogo, na pia Chama hicho kimefanyia kazi kanuni zake, na katika miaka mitano iliyopita, Kamati Kuu ya CPC imetunga au kufanyia marekebisho kanuni 88 za Chama, ikiwa ni asilimia 47 kati ya kanuni zote 188.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako