• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 50 wauawa kwa kupigwa risasi nchini Marekani

  (GMT+08:00) 2017-10-02 19:24:37

  Watu wasiopungua 50 wameuawa na wengine 200 kujeruhiwa kwa kupigwa risasi katika mji wa Las Vegas magharibi mwa Marekani.

  Shambulizi hilo limetokea wakati watu walipokuwa kwenye tamasha la muziki karibu na hoteli ya Mandaley Bay. Polisi wamefunga barabara zote, na kumwua mshambulizi mmoja papo hapo, na kusema wanaamini hakuna washambulizi wengine. Hata hivo polisi wamewataka watu wasiende mahali shambulizi lilipotokea, wala kutotangaza operesheni yao kupitia mtandao wa Internet, ili kuondoa hatari zaidi.

  Baadhi ya ndege zilizokuwa zikielekea Las Vegas pia zimebadilisha njia na kwenda kwenye viwanja vingine kutokana na shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako