• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kukaa kwa muda mrefu ofisini kuongeza hatari ya kupata saratani ya utumbo mpana

  (GMT+08:00) 2017-10-02 19:33:56

  Utafiti mpya uliotolewa na watafiti wa Australia umeonesha kuwa kukaa kwa muda mrefu ofisini kunaongeza hatari ya kupata saratani ya utumbo mpana, hivyo watafiti wanapendekeza watu kupunguza hatari hiyo kupitia mazoezi.

  Mtafiti wa ngazi ya juu wa chama cha saratani cha Victoria cha Australia amesema, utafiti umeonesha kuwa hatari ya kupata saratani ya utumbo mpana ya watu wanaokaa kwa muda mrefu ofisini itaongezeka kwa asilimia 33. Kwenda na kurudi kazini kwa miguu au baiskeli ama kufanya mazoezi ofisini kutapunguza hatari hiyo.

  Kukaa kwa muda mrefu pamoja na mambo mengi yanayohusiana na hatari ya saratani ikiwemo kiwango cha uzito, hali ya uvutaji wa sigara, kiwango cha unywaji wa pombe zinaweza kuathiri hali ya afya. Anayekaa kwa muda mrefu anakabiliwa na hatari kubwa zaidi kuliko wanaopenda kufanya mazoezi. Lakini kukaa kwa muda mrefu si jambo linalosababisha hatari kubwa ya saratani. Kama tunavyofahamu, uvutaji wa sigara unasababisha hatari kubwa ya saratani ya mapafu, lakini kukaa kwa muda mrefu hakujafika kiwango hicho.

  Theluthi moja ya saratani zinaweza kukingwa kupitia mtindo wa maisha unaofaa kwa afya, kama vile kufanya mazoezi, kula chakula kinachofaa kwa afya, kutovuta sigara na kupunguza unywaji wa pombe..

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako