• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Sonko aondoa ada wanazo tozwa wafanyibiashara wadogo

    (GMT+08:00) 2017-10-02 20:24:51

    Wafanyabiashara wadogo mjini Nairobi wamefaidika na kupunguzwa kwa kodi walikuwa wakilipa hapo awali.

    Mwezi Septemba 14 barua ilitumwa kwa maafisa wakuu wa kaunti, na Naibu Gavana Polycarp Igathe kuondoa ada zinatozwa wafanyibiashara wadogo.

    Wafanyibiashara wanaofanya biashara zao nje ya katikati mwa jiji hawata tozwa ada yeyote, kinyume na hapo nyuma walipolazimika kulipa Sh30 kila siku.

    Pia Wasafirishaji mchanga, mbolea na wale wanapakuwa bidhaa kwa kila safari pia wataponea malipo waliokuwa wakilipa kila siku sh500.

    Malipo ya kila wiki kwa maduka madogo ambayo ilkuwa sh 250 pia imefutiliwa mbali, lakini wamiliki wa maduka hayo wanahitajika kuchukua kibali cha kuwaruhusu kufanyabishara hiyo.

    Naibu gavana amesema kuwa ada na malipo inayopaswa kukusanywa ni zile za vifaa vya ujenzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako