• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Nguo za Tanzania zaendelea kupata soko Marekani

    (GMT+08:00) 2017-10-03 18:22:01

    Kampuni ya Tanzania, Tooku Garment Co Ltd inayotengeneza bidhaa za jeans aina ya Levism, Wrangler na The Children Place zinazouzwa nchini Marekani kupitia Mkataba wa Kutoa Fursa za Ukuaji wa Kibiashara kwa Nchi za Afrika (AGOA), imeendelea kuuza kwa wingi nguo zake na bado ina soko la kutosha la bidhaa hizo.

    Kampuni hiyo iliyopo chini ya Mamlaka ya Maeneo Maalumuya Uwekezaji Tanzania (EPZA) eneo la Mabibo External, Dar es Salaam, kwa sasa inazalisha jumla ya nguo za jeans 18,000 kwa siku ambazo kwa mujibu wa mahitaji, bado hazilitoshelezi soko hilo.

    Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho katika eneo la EPZA jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Rigobert Massawe, alikiri kuwa kampuni hiyo inapata oda kubwa ya kusafirisha bidhaa hizo kupitia soko hilo la AGOA.

    Hata hivyo, alibainisha kuwa pamoja na kupata soko hilo kubwa bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi na hivyo kushindwa kuzalisha kwa kiwango kinachohitajika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako