• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Okwi kuongoza Uganda dhidi ya Madagascar, huku Tanzania  kuikabili Malawi

    (GMT+08:00) 2017-10-04 08:58:28
    Timu ya taifa ya Uganda, Uganda the Cranes leo jioni itakutana na timu ya taifa ya Madagascar katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika kwenye uwanja wa Mandela uliopo Nambole mjini Kampala Uganda ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa kufuzu kombe la dunia mwakani nchini Urusi dhidi ya Ghana.

    Emmanuel Okwi mshambuliaji mahiri ataongoza kikosi cha timu yake ya Uganda Cranes. Nayo timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarjia kukutana na timu ya taifa ya Malawi oktoba 7 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa, huku nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta tayari ameshawasili jijini Dar kwa mechi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako