• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiungo wa Real Madrid kukosa mechi 2 kutokana na kuwa majeruhi

    (GMT+08:00) 2017-10-04 08:59:17
    Gkiungo wa kutegemewa wa Real Madrid Gareth Bale hatacheza mechi 2 za kufuzu fainali za kombe la dunia ambazo Wales itapepetana na Georgia kabla ya kuivaa Jamhuri ya Ireland.

    Kiungo huyo wa pembeni wa Real Madrid atakosa mechi hizo, baada ya kupata maumivu ya misuli wiki iliyopita. Mbali na kukosa mechi za kimataifa, mchezaji huyo pia atakosa mchezo wa ligi Kuu Hispania dhidi ya Espanyol.

    Fainali za Kombe la Dunia zimepangwa kuchezwa mwakani nchini Russia na timu mbalimbali zinachuana kuwania tiketi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako