• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaadhimisha sikukuu ya mbalamwezi

    (GMT+08:00) 2017-10-04 18:54:14

    Tarehe 4 ni sikukuu ya jadi ya kichina ya mbalamwezi. Watu wa China wamefanya shughuli mbalimbali ili kuadhimisha siku hiyo.

    Katika sikukuu hii ya mbalamwezi wachina hula keki ya mwezi pamoja na watu wote wa familia. Kwenye maduka maarufu ya keki ya mwezi mjini Shanghai, wateja wamefika asubuhi na mapema.

    "Nilifika saa nne asubuhi, nimesubiri kununua keki za mwezi zaidi ya saa tatu."

    "Mimi natoka mji mwingine, napenda keki za mwezi zilizotengenezwa na duka hili."

    Huko Tianjin, ambao ni mji muhimu ya bandari kaskazini mwa China, maonesho ya vifaa vya kutengenezea keki za kijadi yamefanyika. Baadhi ya vifaa hivyo vilitengenezwa miaka mia mbili iliyopita, licha ya zile zilizotengenezwa nchini China, baadhi ya vifaa vinatoka Japana na peninsula ya Korea. vifaa hivyo vilivyotengenezwa kwa malighafi za ubao, chuma, udongo au mawe vina michoro ya malaika wa Chang'e, sungura na kasri ya mwezi, ambayo yote inatokana na hadithi ya jadi ya kichina, na inaashiria mambo mazuri kama vile maisha bora, maisha marefu, usalama, utulivu na kuwa na watoto wengi.

    Bw. Wang Laihua anapenda kukusanya na kuhifadhi vifaa vya kutengeneza keki za jadi. Anasema madhumuni ya maonesho hayo ni kutangaza na kueneza utamaduni wa jadi wa kichina.

    "Kivutio zaidi cha vifaa hivyo ni michoro. Michoro ni alama ya utamaduni. Michoro kwenye mitambo ya kutengeneza keki za jadi ni baraka."

    Sikukuu ya mbalamwezi iliyoanza miaka zaidi ya 1,300 iliyopita pia inajulikana kama sikukuu ya kuabudu mwezi. Katika zama za kale, wakati wa sikukuu hiyo, wachina hufanya sherehe kubwa ya kuabudu mwezi. Katika tamasha la kijadi la sikukuu ya mbalamwezi la ukuta mkuu wa Shiguang lililoandaliwa na kijiji cha Shixia wilaya ya Badaling, mjini Beijing, watalii wanaweza kuona sherehe hiyo ya kijadi. Mwandaaji wa tamasha hilo Bi He Yuling ameeleza kuwa kwa mujibu wa mila na desturi, sherehe hiyo inaendeshwa na wanawake, kwani malaika anayeishi kwenye mwezi ni mwanamke.

    Miji ya Nanjing na Fuzhou iliyoko kusini mwa China pia imefanya shughuli za kuabudu mwezi, ili kuomba baraka kutoka mungu.

    Mbali na China, baadhi ya nchi za Asia ya mashariki pia zinasherehekea sikukuu ya mbalamwezi. Mwenyekiti wa shirikisho la kuhifadhi mabaki ya mali za urithi za utamaduni la mji wa Shenzhen Bw. Wang Chengtai anasema,

    "Watu wanafanya shughuli mbalimbali ili kuadhimisha sikukuu ya mbalamwezi. Sikukuu hiyo pia ilipokelewa na nchi nyingine zilizoko karibu na China, kama vile Korea ya Kusini, Korea ya Kaskazini na Japan."

    Wachina wanapenda kukutana na wanafamilia wakati wa sikukuu ya mbala mwezi. Mwaka huu, sikukuu hiyo imekwenda sambambam na mapumziko ya wiki moja ya siku ya kitaifa. Hivyo wachina wengi wamekwenda kutalii pamoja na watu wa familia. Idara kuu ya utalii ya China inakadiria kuwa katika siku hizo za mapumziko, idadi ya wachina watakaotalii nchini China na katika nchi za nje itazidi milioni 700.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako