• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwekezaji wa klabu ya Arsenal akanusha kuuza hisa kwa mwekezaji mwenzake

    (GMT+08:00) 2017-10-05 08:21:48

    Mwekezaji wa pili kwa ukubwa katika klabu ya Arsenal, Alisher Usmanov, amesema hajafanya mazungumzo yoyote na mwenye hisa mkuu wa klabu hiyo Stan Kroenke kuhusu kumuuzia kiwango chake cha hisa katika klabu hiyo. Imeripotiwa kuwa Kroenke ambaye anamiliki asilimia 67 za hisa aliwasilisha ombi la kutaka kununua hisa za Usmanov ambazo ni asilimia 30.

    Hatahivyo Usmanov mwenye umri wa miaka 64 amesema kuwa maslahi yake katika Arsenal ni ya muda mrefu. Licha ya kumiliki hisa katika klabu hiyo Usmanov hayupo katika bodi ya klabu hiyo ambayo hufanya maamuzi na amekuwa akimlaumu Kroenke kwa matokeo mabaya ya Arsenal uwanjani. Raia huyo wa Uzebek aliwasilisha ombi la pauni bilioni moja mnamo mwezi kuinunua klabu hiyo lakini likakataliwa na Kroenke.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako