• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Atletico Madrid kuwapatia mashabiki wa FC Barcelona tiketi kinyume na matakwa ya Barca

    (GMT+08:00) 2017-10-06 09:06:12

    Klabu ya Atletico Madrid imesisitiza kuwa itawapatia FC Barcelona tiketi kama wanavyofanya kwa timu nyingine za La Liga. Hii imekuja baada ya wafalme hao wa soka ya Hispania Barcelona kuitaka timu hiyo kutowapatia tiketi mashabiki wao kwa kuhofia kuchomoza vitendo vya vurugu kutokana na maswala ya kudai Jimbo la Catalonia kujitoa Hispania. Atletico imesema kuwa imetoa tiketi za ugenini sawa na timu nyingine za La Liga msimu huu.

    Barca imepatiwa tiketi 250, kwaajili ya mchezo huo utakaofanyika Oktoba 14 katika dimba jipya la Wanda Metropolitano. Ambapo wamesema hiyo ni sawa na kiasi cha tiketi walichoipatia timu ya Sevilla na Malaga katika michezo ijayo itakayo pigwa katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua idadi ya watu 68,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako