• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utafiti waonesha kuwa ukosefu wa usingizi unaweza kuathiri afya ya kiakili na uwezo wa kumbukumbu

  (GMT+08:00) 2017-10-10 08:11:40

  Ukosefu wa usingizi huwafanya watu kujisikia uwezo wao umepungua. Utafiti mpya uliotolewa na Chuo kikuu cha Leeds umeonesha kuwa ukosefu wa usingizi unaweza kuathiri afya ya kiakili na uwezo wa kumbukumbu.

  Watafiti wa Chuo hicho walishirikiana na kampuni moja kufanya utafiti mkubwa uliowashirikisha watu zaidi ya elfu moja wa Uingereza wenye umri kutoka miaka 18 hadi 80. Watafiti waliwataka watu hao kujaza fomu kuhusu tabia za kulala, uwezo wa kumbukumbu, hali ya kisaikolojia na hali ya maisha, na kutafiti matokeo ya takwimu hizo.

  Watafiti wamesema, kutokana na takwimu, ukosefu wa usingizi una uhusiano mkubwa na kushuka kwa afya ya kiakili na kuwa mbaya kwa uwezo wa kumbukumbu, haswa kwa wale wanaolala kwa muda usiozidi saa tano, uhusiano huo utakuwa mkubwa zaidi. Kwa mfano wanaweza kusahau jukumu wanalotakiwa kufanya, kusahau mahali ambako jambo lilitokea au kusahau jambo walilopanga.

  Hivi sasa mfumo wa afya ya umma wa Uingereza umependekeza watu wazima kulala saa 7 hadi 8 kila usiku.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako